Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akifunga mafunzo maalum ya kijeshi kwa ajili ya kupambana na ujangili
kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida
hivi karibuni.
Askari
wanyamapori wakionesha kwa vitendo namna ya kupambana na majangili
wakati wakiwakamata majangili wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Balozi
wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress akizungumza wakati wa
kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana na ujangili kwa Askari
wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida hivi karibuni.
Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za
kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na
kukabiliana na majangili.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania ( TAWA) Bw. Martin
Loibook akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Pori la Akiba
la Rungwa mkoani Singida hivi karibuni.
Askari
wanyamapori wakionesha kwa vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu
yaliyofanyika katika Pori la Akiba la Rungwa Mkoani Singida
yaliyohitimishwa hivi karibuni wakionesha namna ya kupambana na
majangili wakati wakiwakamata majangili.
---------------------------------------------------------------
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi
ametoa wito kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili waache kazi
hiyo mara moja na badala yake watafute kazi nyingine zitakazoweza
kuwapatia kipato halali kwa kufanya hivyo wataweza kujiepusha kutiwa
nguvuni na askari wanyamapori waliobobea kwa kazi hiyo.
Maj. Gen Milanzi alitoa wito huo hivi
karibuni wakati wa akifunga mafunzo maalumu ya kupambana na Ujangili
kwa askari wanyamapori katika pori la akiba la Rungwa mkoani Singida
yaliyofadhiliwa na Marekani na yaliyotolewa na Kikosi maalum cha
wanajeshi kutoka Marekani.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu
sana kwa askari wanyamapori ili kuendelea na kukabiliana na wimbi kubwa
la ujangili kwa kuwa majangili wasasa wanatumia silaha za kisasa tofauti
na majangili wa zamani ambao walikuwa wakitumia upinde na mishale.
Aliongeza kuwa majangili wa sasa
ambao askari wanyamapori wamekuwa wakikabiliana nao maporini ni wale
ambao wanatumia silaha za kivita hiyo ni lazima askari wetu wapewe
mafunzo ya hali ya juu ili waweze kukabiliana nao.
Aidha Katibu Mkuu, Milanzi alisema
Wizara imejipanga kuhakikisha suala la ujangili linakwisha ambapo kituo
kingine cha mafunzo ya kijeshi kwa askari wanyamapori cha Mlele
kilichopo Mkoani Katavi kimeanzishwa mbali na vyuo vya Pasiansi na
Mweka, Likuyu Sekamaganga ambavyo pekee ndivyo vilivyokuwa vikitoa
mafunzo kwa askari wanyamapori.
Aliongeza kuwa, kwa sasa Serikali
imejipanga kwa kushirikiana na Interpol kuhakikisha kuwa hatakamatwa
jangili tu aliyehusika kuua mnyama porini bali mtandao wote utakamatwa
na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria mahali popote.
Akizungumza na wahitimu wa mafunzo
hayo, Milanzi alisema mafunzo hayo yamejikita kuwasaidia kupambana na
majangili, magaidi pamoja na majambazi ambapo wao ndo watu wa kwanza
kukumbana nao wakiwa porini kwani ndiko wanakotumia kujificha kwahiyo
ujuzi walioupata umewaongezea ufanisi katika kulinda maliasili zilizopo
kwenye maeneo yao.
Aliwataka pia wahitimu hao kufanya
kazi kwa kujituma wasiishie tu kusherekea kumaliza mafunzo bali
waonyeshe kwa vitendo hii itasaidia na kuipa ari Marekani pamoja na
Asasi za kimataifa zenye lengo la kusaidia nchi katika vita dhidi ya
Ujangili.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani
nchini Tanzania, Mark Childress amewataka wahitimu wazingatie mafunzo
waliyopata kwa kuyafanyia kazi ili Pori la Akiba la Rungwa liwe sehemu
salama kwa wanyamapori wanaopatikana katika pori hilo.
Ameahidi kuwa nchi yake itaendelea
kuisaidia Tanzania kwa kuwa suala la ujangili bado ni kubwa linalohitaji
ushirikiano wa pande zote ili liweze kutokomezwa
0 comments:
Post a Comment