Waziri wa wizara ya Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe
atembelewa na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida
akiwa ameongozana na Rais wa Shirika la AFRECO la Japan Bw. Tetsuro
Yano kuzungumza namna gani serikali ya Japan kupitia Shirika hilo
wanaweza kuchangia maendeleo ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na
Utalii
Katika mazungumzo hayo
hivi karibuni , Prof. Maghembe amemuomba kuchangia katika kuimarisha
Utalii katika nyanja tofauti ikiwemo kwa kusaidia kupambana na majangili
kupitia kitengo maalumu cha kupambana na ujangili kwa kuwawezesha na
vifaa mbalimbali kama vile magari vitakavyosaidia kuamaliza suala la
ujangili.
Pia, aliomba
Japan isaidie katika kuhimiza nchi mbalimbali ikiwe China katika kuacha
kuagiza meno ya tembo ilikuuwa soko zima la ujangili.
Aidha,
alimuomba kuhimiza wawekezaji waliopo Japan kuja nchini kujenga hoteli
zenye sifa ya nyota tano katika maeneo ya fukwe za bahari ambako
wanatarajia kukuza utalii wa fukwe hizo za bahari.
Aliongeza kuwa
wawekezaji wote wa ndani na nje ya Tanzania wanakaribishwa na wale
watakaokidhi sifa zinazohitajika ndio watakaoruhusiwa kujenga kwenye
fukwe hizo.
Naye , Bw. Tetsuro Yano ambaye ni Rais wa Shirika la
AFRECO amekubaliana na maombi ya Waziri wa Maliasili na Utalii , Prof
Maghembe kuwa suala la uhifadhi ni suala la kidunia hivyo kwa
kushirikiana na nchi yake wataweza kushiriki kwenye vita dhidi ya
ujangili kwa kuisaidia Tanzania katika kutoa vifaa vya kisasa
Naye, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida aliahidi
kuwa ataendelea kuwahimiza wawekezaji kutoka nchini Japani pamoja na
serikali ili waweze kuwekeza katika masuala ya Utalii na hivyo
kuchangia katika kukuza maendeleo ya wizara hii
WAZIRI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII PROF JUMANNE MAGHEMBE AWATAKA WAJAPAN WAJE KUWEKEZA NCHINI KWENYE UTALII.
Tuesday, September 13, 2016
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment