Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland ya Uingereza katika uzinduzi
wa utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na uhamasishaji wa uwekezaji na
maendeleo ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development).
Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29
Novemba, 2014 kwenye kiwanja cha “Stadium of Light”, kinachomilikiwa na
Sunderland Association Football Club (SAFC)
Tukio hilo lilihudhuriwa na Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe, Maafisa waUbalozi wa
Tanzania nchini Uingereza, Watanzania waishio nchini Uingereza pamoja na baadhi
ya maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania
Wakati wa uzinduzi huokatikakingo zakuta
za uwanja yalionekana matangazo
yanayotangaza vivutio vya utalii vya
Tanzania ambapokulikuwa na mechi kati ya timu ya Sunderland na Chelsea FC iliyorushwa
moja
kwa moja na kituo kinachorusha mechi
mbalimbali za mpira wa miguu cha DSTV.
Aidha wachezaji wa timu ya Sunderland
walionekana wakiwa wamevaa jezi maalum zilizoandikwa ‘Visit Tanzania’ wakati
wakifanya mazoezi kabla ya mechi hiyo.
Bodi yaUtalii Tanzania imetumia
fursa yamechi hiyo kuhamasisha wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya Uingereza
pamoja na mashabiki wa Timu hizo wa nchi zote duniani kutembelea vivutio vya
utalii wa Tanzania
Imetolewa na
BODI YA UTALII TANZANI
01/12/2014
0 comments:
Post a Comment