UINGEREZA YATOA SH. BILIONI 27 KUPAMABANA NA UJANGILI.

Serikali ya Uingereza imetioa doala milioni 15 (sawa n ash. Bilioni 27), ikiwa ni sehemu mchango wa kukabiliana na vitendo vya ujangili na mauaji ya wanyamapori nchini.
Mchango huo ni kuunga jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuokoa maisha ya wanyamapori katika hifadhi ambao wamekuwa wakiuawa na majangili.
Pia nchi ya Uingereza kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la kupinga ujangili wa meno ya tembo la ‘’STOP IVORY’’na Tanzania zimetiliana saini mkataba wa makubaliano ya mapambano ya kukomesha ujangili wa wanyamapori hasa ujangili wa meno ya tembo unaofanywa hapa nchini.
Akizungumza hivi karibuni Mpingo House jijin Dar es Salaam, Waziri ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema hatua hiyo ya kusaini makubaliano kati ya Uingereza na Tanzania itaisaidia kulinda na kuhifadfhi wanyamapori ambao wamekuwa wakiwindwa kila kukicha na majangili.
Mhe. Nyalandu alisema hatua hiyo itasaidia sekta ya Utalii kukua kwa kuwa pesa hizo zitasaidia kutokomeza ujangili na hivyo kuweza kuongeza pato la utalii kwa kuwa Utalii wa wanyamapori ndio unaotegemewa kwa kiasi kikubwa.
‘’Nafarijika sana kuona marafiki zetu Uingereza wameguswa na jitihada zinazofanywa na serikali yetu katika vita dhidi ya Ujangili huu ni mfano wa kuigwa na mataifa mengine makubwa kutuunga mkono katika kampeni hii.’’ Mhe. Nyalandu alisema.
Aidha ameipongeza Jamhuri ya watu wa China kutangaza nia yao ya kusitisha kujihusisha na usafarishaji wa bidhaa za meno ya tembo kutoka Afrika.
‘’ Hatua hii ya China inatoa mwaya kwa mataiafa mengine makubwa duniani yanayohitaji bidhaa ya meno ya tembo kuacha mara moja kama China ilivyofanya hii itaweza kunusuru tembo wa Afrika ‘’ Mhe. Nyalandu alisisitiza
Kwa Upande wa Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, alisema kuwa anaipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada iliyoonesha kukabiliana na vitendo vya ujangilini nchini na hii ndio sababu iliyowavutia wao kutoa pesa ili kuongeza nguvu katika vita hivyo.
Alisema kwamba Serikali ya Uingereza itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutokomeza vita dhidi ya Ujangili ikiwa ni pamoja na kuendelea kuyashawishi mataifa makubwa yanayojihusisha na ununuzi wa bidhaa ya meno ya tembo kuachana na biashara hiyo.
Dianna alisema vita dhidi ya Ujangili wa Wanyamapori ni lazima upigwe vita duniani kote ikiwa ni jitihada ya kuokoa tembo amabao wamekuwa wakiuawa kwa ajili ya meno ya tembo na hivyo sekta ya Utalii kudorora.
‘’Tutaendelea kuunga mkono katika kukabailiana na vitendo vya Ujangili kwa kuwa wanyamapori ni urithi wa dunia’’ Dianna alisisitiza.
CHANZO: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII TANZANIA


0 comments:

Post a Comment