Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi
( kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Deogratius Mdamu
(kushoto) wakimsikiliza Mjumbe ( hayupo pichani ) wakati wa Mkutano
wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC)
uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar es Salaam akiwa anazungumzia
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini na kutoa
ushauri ya namna kuuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa bado ni
changamoto kwa wananchi wengi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo
nchini
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi akisisitiza jambo wakati alipokuwa anamkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi kufungua Mkutano Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika jana Mpingo House jijini Dar es Salaam wa kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) wakiwa wanajadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini kwa kutoa maoni, ushauri na ufumbuzi wa changamoto ikiwa na kuchangia mikakati mbalimbali itakayowezesha kusaidia kuhamasisha Utalii wa ndani.
Wakati nchi nyingi Afrika zikiwa zinafanya jitihada mbalimbali za
kuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa ndo wa uhakika katika
kuiingizia nchi mapato hata pale majanga yanapotokea, Nayo Tanzania
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuhakikisha kuwa
Utalii wa ndani unakua kwa kasi inayotarajiwa.
Baadhi ya Majanga
hayo yanayoathiri Sekta ya Utalii ni milipuko ya magonjwa kama Ebola,
matukio ya Ugaidi Kenya na kushuka kwa Euro ya Ulaya dhidi ya Dola ya
Marekani.
Hivyo Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana
na Wadau wa Utalii nchini wamepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa
Utalii wa ndani unakuwa tegemeo tofauti na sasa ambapo Watalii kutoka
nje ndio wamekuwa wamekuwa wakitembelea hifadhi zetu kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ijulikanayo
kama Tourism Facilitation Committee ( TFC) uliofanyika jana Mpingo
House jijini Dar esSalaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja.
Generali. Gaudence Milanzi na Utalii amesema maendeleo ya Utalii
yanahitaji sana Utalii wa ndani kuimarika baadala ya kudhani kuwa
vivutio vya utalii vilivyopo ni kwa ajili ya wageni kutoka nchi za nje.
Meja. Generali. Milanzi amesema Utalii ni sekta nyeti sana katika
kuliingiza Taifa pesa za kigeni lakini hata hivyo ni sekta ambayo
imekuwa inaathirika kwa haraka sana pindi majanga yanapotokea nchi
jirani hivyo ni lazima jamii ijengewe utamaduni wa kutembelea vivutio
vya Utalii ili kuweza kujihakikishia Watalii wa ndani wanakuwa wengi.
Baadhi ya mikakati iliyopendekezwa na Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji
Utalii (TFC) ni kuwawezesha maafisa Utalii wa Halmashauri
wanatengewa bajeti ya kutosha, wanajengewa uwezo kuhusu ya vivutio vya
utalii vilivyopo kwenye maeneo yao pamoja na Idara ya Utalii kufungua
ofisi kila kanda ili kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Aidha,viwanja vya ndege vilivyopo nchini viimarishwe ikiwa pamoja na
nchi kuwa ndege zake kama ilivyo kwa nchi jirani kama Kenya na Rwanda
Awali , Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi alisema
Mkutano wa TFC hutoa fursa za kuziibua na kujadili changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii hivyo Sekta Binafsi zinawajibu
mkubwa wa kuhakikisha changamoto zinazoikabili sekta zinatafutiwa
ufumbuzi
Aliongeza kuwa Idara ya Utalii imekuwa ikishiriki
katika maonesho mbalimbali ya kitaifa lengo likiwa ni kutoa elimu kwa
jamii kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya Utalii nchini.
Aidha, Prof Wineastor Anderson amesema sekta ya Utalii imekuwa inakua
lakini si kwa kiwango cha kuridhisha hivyo jitihada za kutangaza utalii
ndani na nje nchi upewe uzito unaostahili kwa kuiwezesha Bodi ya
Taifa ya Utalii inatengewa bajeti ya kutosha.
Wakati huo huo,
Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania ( TCT) Bw.
Richard Rugimbana, amesema Utalii wa ndani ili uweze kukua suala la
elimu linahitajika kutolewa ili kuweza kuibadilisha jamii ipende
kutembelea vivutio vya Utalii.
Naye Kamanda wa Polisi (ACP)
Ndaki anayeshughulikia dawati la Utalii ( Tourism Police Unit)
amewahakikishia usalama watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea
vivutio vya Utalii bila kuwa na hofu yoyote kwa kuwa Jeshi la Polisi
nchini lipo macho muda wote.
0 comments:
Post a Comment