Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe
amepongeza jitihada zinazofanywa na watafiti kwa kurudisha mbwa mwitu
katika Hifadhi ya Taifa Serengeti baada ya kutoweka katika miaka ya
tisini. Waziri Maghembe alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipokuwa
akiachia huru kundi la sita la mbwa 17 waliokuwa wamehifadhiwa katika
boma maalum ili kurejea katika makazi yao ya asili.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa
Jumanne Maghembe (MB) akisalimiana na Mhifadhi Ashery Loishooki mara
baada ya kuwasili katika eneo la Nyasirori, Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kwa ajili ya kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11
waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita katika boma maalumu la mradi wa
mbwa mwitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof.
Jumanne Maghembe (MB) akiongea wakati wa tukio la kuachia huru kundi
la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye
boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Waziri wa Maliasili an Utalii akiongea jambo wakati wa tukio la kuachia huru kundi
la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye
boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof.
Jumanne Maghembe (MB) akielekea katika boma la mbwa mwitu kwa ajili ya
tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa
wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Wanahabari wakichukua picha mbalimbali wakati mbwa mwitu walipokuwa wakitoka kwenye boma.
Kundi la sita la mbwa mwitu 11 wakitoka katika boma maalum katika Hifadhi ya Serengeti.
Mbwa mwitu sasa wako huru baada ya kuachiwa katika boma.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiongea na wanahabari mara baada ya tukio la kuachiwa kwa mbwa mwitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.
Jumanne Maghembe (MB) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti.
Profesa Maghembe amesema serikali itaendelea kuwekeza katika
eneo la utafiti ili kuwezesha sekta ya uhifadhi nchini kuwa na mchango
mkubwa katika uchumi wa taifa. Alisema mabadiliko ya tabia nchi
yameathiri sekta nyingi ikiwemo ya uhifadhi na kuwa wanyama wamekuwa
wakiathirika na mabadiliko hayo hivyo ni vema uwekezaji mkubwa
ukafanyika katika eneo la utafiti ili kujua namna ambavyo uhifadhi
unaweza kukabiliana na mabadiliko hayo.
Mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu unalenga kurudisha mbwa mwitu
katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao walitoweka kabisa tangu
mwaka 1994 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kubainika kisayansi.
Mradi huu unasimamiwa na kuendeshwa na watafiti wa kitanzania.
Tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2011, jumla ya makundi sita
ya mbwa mwitu wamesharudishwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti. Makundi
haya ni pamoja na Vodacom ambapo Kampuni hii ya simu ilifadhili gharama
za mradi; Serengeti; Loliondo; Kikwete; Nyasirori na hili la mwisho
ambalo lilipewa jina la Markus Borner, mwanasayansi kutoka nchini
Ujerumani aliyetumia miaka 35 akifanya shughuli za uhifadhi katika
hifadhi ya Serengeti.
Mradi wa mbwa mwitu Serengeti unaendeshwa na Taasisi ya
Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,
TANAPA na Chuo Kikuu cha Glasgow.
Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa
Hifadhi za Taifa
0 comments:
Post a Comment