Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof.Jummane Maghembe ( kushoto) akisisitiza
jambo wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini
Dare salaamu wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kuwasimamisha kazi
Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS), kulia ni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani
Baadhi
ya Waandishi wa habari walioalikwa kwenye mkutano na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakiandika taarifa za
Wakurugenzi kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ili uweze kufanyika
kutokana na makusanyo dni ya maduhuli yatokanayo na mazao ya misitu
nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Mghembe amemsimamisha
kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini, (TFS) Bw.
Juma Mgoo pamoja na Wakurugenzi wawili wa wakala hiyo ili kupisha
uchunguzi kutokana na ukusanyaji usioridhisha wa mapato yatokanayo na
mazao ya misitu.
Prof. Maghembe ametaja majina ya Wakurugenzi
hao aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkurugenzi Rasilimali Misitu, Bw.
Zawadi Mbwambo pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi
endelevu ya Misitu, Bw. Nurdin Chamuya
Wengine waliosimamishwa
kazi ni wakuu wa Kanda za Wakala wa Huduma za Misitu nchi nzima
ambao ni Bw. Hubert Haule wa Kanda ya Kusini, Bw. Bakari Rashidi wa
kanda ya Mashariki, Bw. Shabani Mwinyi Juma wa kanda ya
kati , Emanuel Minja wa kanda ya Magharibi pamoja na Bw. Bruno wa
nyanda za juu kusini
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Makao
Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, Prof. Maghembe amesema
hatua hiyo imekuja baada ya kubaini shehena kubwa za magogo aina ya
mninga katika Mkoa wa Rukwa wilayani Kalambo yakiwa yamekatwa na
kuwekwa ndani ya makontena kule kule ndani ya msitu pamoja na
kutengenezewa nyaraka feki zinazoonesha magogo hayo yanatoka nchini
Zambia tayari kwa kusafirishwa kupelekwa nchini China lakini hata
hivyo baada ya kubaini wizi huo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na
Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania ( TFS).
Amesema kuwa baada ya
kubaini hivyo usiku wa jana aliweza kupata taarifa kuwa shehena ya
Magogo hayo yenye thamani ya shilingi milioni 500 yaliyotakiwa
kupelekwa Makao makuu ya Wilaya ya Kalambo yamemwagiwa petrol na
yamechomwa moto
Aliongeza kuwa kumekuwa na ubadhilifu unaofanywa
na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali yanayotokana na
rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa katika
mfuko Mkuu wa Serikali.
Kwa upande mwingine , Prof Maghembe
amesema kuwa pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi
benki kwa wakati na hata zikipelekwa benki zimekuwa zikipelekwa pungufu
na muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.
Wakati
huo huo, Waziri Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Wanyamapori wa Matumizi Endelevu, Dkt. Charles Mulokozi kwa
kosa la kukaidi agizo la kusaini vibali vya kusafirisha Wanyamapori nje
ya nchi.
Hatua hiyo imekuja baada ya jana nyani 61 kukamatwa
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na kubaini kuwa Idara
ya Wanyamapori ndio iliyotoa vibali vya kusafirisha nyani hao na
vibali hivyo vikiwa vimetiwa saini na Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa ndege ya kutoka Ulaya Kusini iliyotakiwa kusafirisha nyani hao imeshikiliwa pamoja na rubani wake kwa mahojiano zaidi.
Ameongeza kuwa ndege ya kutoka Ulaya Kusini iliyotakiwa kusafirisha nyani hao imeshikiliwa pamoja na rubani wake kwa mahojiano zaidi.
Prof
,Maghembe amesema kutokana taarifa alizozipata kuwa jumla ya nyani 450
ndio waliokuwa wanawindwa kwa ajili ya kusafirishwa kupelekwa nje.
0 comments:
Post a Comment