Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Ngorongoro
jana. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Eng. Angelina Madete.
-----------------------------------------------------------------
SERIKALI
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepanga kuboresha na kuimarisha
vivutio vya utalii wa ndani ikiwemo fukwe na bahari na huduma za hoteli
za kitalii nchini ilikuhakikisha kuwa Wizara hiyo inavuka lengo la
ukusanyaji wa mapato.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Mhandisi RamoMakani wakati wa mkutano na waandishi wa
habari akizungumzia fursa na mchango wa sekta ya utalii katika kukuza
uchumi wa taifa.
Alisema lengo la uboreshaji wa huduma hizo ni kufikia utekelezaji na wa Mipango ya Sekta ya Maliasili na Utalii katika kuchangia kuongezeka kwa pato la taifa hatimaye kukuza uchumi wa nchi.
“kuna haja ya kuboresha, kuongeza nguvu na kuimarisha kila hitaji ili
kuwezesha sekta ya Maliasili na Utalii kuzalisha zaidi ili kuchangia
pato la taifa na hatimaye kukuza uchumi wa Taifa “ alifafanua Mhandisi
Makani.
Pia alisema kuwa Wizara inalenga kuboresha utangazaji wa vivutio,
bidhaa, na huduma, kuboresha miundombinu ndani ya hifadhi, kuhifadhi
vivutio na mazingira yake, kuboresha utoaji wahuduma pamoja na
kuendeleza vivutio vilivyopo na kuanzisha vivutio vipya.
Akizungumza kuhusu uboreshwaji wa utalii wa ndani Mhandisi Makani alisema utalii huo ukiimarishwa mapato yake
yatalingana na mapato yanayokusanywa kutoka kwa watalii wa nje kwani
kwa sasa wananchi wana mwamko mkubwa wa kutembelea vivutio vilivyopo
hapa nchini.
“Tukiimarisha
utalii wandani mapato yake yatalingana na mapato yanayokusanywa kutoka
kwa watalii wa nje, kwa mfano idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi ya
kisiwa cha Saa imeongezeka hadi kufika asilimia 94.5 kwa mwaka
2015/2016″ aliongeza Mhandisi Makani.
Kwa mujibu wa Mhandisi Makani alisema katika kuboresha hudumu za
utalii, sekta hiyo bado haijaimarika kutokana na ukosefu wa ujuzi wa
baadhi ya watoa huduma na hivyo kupelekea upungufu wa kiwango cha
watalii.
Mhandisi
Makani alisema Wizara imeandaa Semina itakayofanyika kikanda nchini
kote kwa ajili yakuwawezesha vijana kupata elimu juu ya utoaji wa
huduma stahiki zinazohusu sekta ya
utalii.
Waziri huyo alisema kuwa Wizara itasimamia kwa ukaribu taratibu nzima
za uanzishwaji wa hoteli pamoja na utoaji wa huduma zitakazokidhi
viwango kwa kutoa Elimu, kusajili nakufanya ukaguzi wa mara kwa mara
katika hoteli hizo.
0 comments:
Post a Comment