WAZIRI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII PROF JUMANNE MAGHEMBE AWATAKA WAJAPAN WAJE KUWEKEZA NCHINI KWENYE UTALII.

Waziri wa wizara ya Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe atembelewa na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa ameongozana na Rais wa Shirika la AFRECO la Japan Bw. Tetsuro Yano kuzungumza namna gani serikali ya Japan kupitia Shirika hilo wanaweza kuchangia maendeleo ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii
Katika mazungumzo hayo hivi karibuni , Prof. Maghembe amemuomba kuchangia katika kuimarisha Utalii katika nyanja tofauti ikiwemo kwa kusaidia kupambana na majangili kupitia kitengo maalumu cha kupambana na ujangili kwa kuwawezesha na vifaa mbalimbali kama vile magari vitakavyosaidia kuamaliza suala la ujangili.
Pia, aliomba Japan isaidie katika kuhimiza nchi mbalimbali ikiwe China katika kuacha kuagiza meno ya tembo ilikuuwa soko zima la ujangili.
Aidha, alimuomba kuhimiza wawekezaji waliopo Japan kuja nchini kujenga hoteli zenye sifa ya nyota tano katika maeneo ya fukwe za bahari ambako wanatarajia kukuza utalii wa fukwe hizo za bahari.
Aliongeza kuwa wawekezaji wote wa ndani na nje ya Tanzania wanakaribishwa na wale watakaokidhi sifa zinazohitajika ndio watakaoruhusiwa kujenga kwenye fukwe hizo.
Naye , Bw. Tetsuro Yano ambaye ni Rais wa Shirika la AFRECO amekubaliana na maombi ya Waziri wa Maliasili na Utalii , Prof Maghembe kuwa suala la uhifadhi ni suala la kidunia hivyo kwa kushirikiana na nchi yake wataweza kushiriki kwenye vita dhidi ya ujangili kwa kuisaidia Tanzania katika kutoa vifaa vya kisasa
Naye, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida aliahidi kuwa ataendelea kuwahimiza wawekezaji kutoka nchini Japani pamoja na serikali ili waweze kuwekeza katika masuala ya Utalii na hivyo kuchangia katika kukuza maendeleo ya wizara hii


0 comments:

Post a Comment