Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro.
Ikumbukwe na Ieleweke hapa ya kwamba Mamlaka ya hifadhi
Ngorongoro si eneo ambalo ni hifadhi ya Taifa na
vile vile eneo hili la ngorongoro halipo chini ya
Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) na badala yake ni
Shirika huru kama jinsi ilivyo TANAPA likijitegemea. Kazi
na majukumu ya TANAPA na NGORONGORO zinafanana katika
kuhifadhi viumbe hai na makazi yake kuwa
endelevu kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo. Lakini
kwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni eneo ambalo ni hifadhi
mseto ambapo kuna viumbe hai aina tatu
vikiishi kwa pamoja ambavyo ni watu ambao
zaidi ni jamii ya Kabila la Wamaasai, mifugo yao
kama vile Kondoo, Mbuzi na Ngombe na tatu ni Wanyamapori.
HISTORIA YAKE:
Sababu ya msingi iliyopelekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni ukweli wa mambo ya kwamba jamii ya Kabila la Maasai ilikuwa ikiishi katika maeneo yote ya Serengeti na Ngorongoro kwa miaka miangi pamoja na na Wanyamapori. Wamaasai ni jamii ya nilotiki ambao asili yao ni Kusini mwa Sudani na ni jamii ya wafugaji kiasili. Kwa kuwa jamii ya Wamaasai ilikuwa ikiishi ndani ya maeneo haya ya uhifadhi pasipo utaratibu maalumu na mwongozo, jamii hii ya kabila la Wamaasai ilikuwa katika janga kubwa la wanyama pori kama vile magonjwa ya maambukizo ya wanyamapori na majanga mengineyo.

Hivyo basi serikali ya Wakoloni Waingereza wakati wa
kipindi hicho iliamua kuanzisha maeneo
mawili tofauti ya uhifadhi. Eneo moja la uhifadhi
litumike maalumu kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori pekee
ambayo ndio Serengeti ya leo hii na vile
vile eneo jingine la uhifadhi litumike kama hifadhi
mseto ambapo wamaasai wenyewe, mifugo yao pamoja na
wanyamapori wakiishi kwa pamoja yaani (conservation).
Hatimaye Wamaasai wote waliokuwa wakiishi
Serengeti ya wakati wa kipindi kile wakahamishiwa Mamlaka ya
hifadhi ya Ngorongoro ya leo hii. Vile vile malengo mengineyo
yalikuwa ni katika kulinda maslahi ya jamii ya kabila la
Wamaasai ambao wameiishi na Wanyamapori pasipo
uharibifu wowote ule kwa miaka mingi. Jamii ya
kabila la wamasai wanachukuliwa kuwa ni
wahifadhi asilia kwa sababu ya kuishi na
wanyamapori kwa muda mrefu kihistoria.
Ikumbukwe na ieleweke hapa ya kwamba
hifadhi za Taifa zote zilizopo chini ya Shirika la
hifadhi za Taifa (TANAPA) pamoja na mamlaka ya hifadhi ya
ngorongoro uanzishwaji wake ulikuwa ni mwaka 1959. Kijiografia,
mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro inapatikana Mkoani Arusha.
MAANDALIZI YA USAFIRI:
Mahitaji ya fedha katika safari yenu ya matembezi hifadhini mamlaka ya Ngorongoro.

KUANZISHWA KWAKE:
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ilianzishwa mnamo mwaka 1959. Hii ilitokana na kumegwa na kutengwa eneo lake kutoka Serengeti na kulifanya eneo hili kuwa ndio hifadhi mseto pekee Tanzania (Conservation) ambapo watu, Wanyamapori na mifugo yao wakiishi kwa pamoja. Sehemu kubwa ya wananchi wanaoishi ngorongoro ni jamii ya kabila la wamaasai.

ENEO LAKE:
Ina ukubwa wa eneo lenye kilomita za mraba 8300 (ambapo ni sawa na maili za mraba 3200). Katika ukubwa wa jumla wa eneo lote, Bonde la ngorongoro (Ngorongoro Crater) ina ukubwa wa kilomita za Mraba zaidi ya 260 au asilimia 3, Msitu wa asili wa nyanda za juu Kaskazini asilimia 20,maeneo mengineyo ya milima asilimia 27,na maeneo ya tambarare ni asilimia 50.

UFIKAJI HIFADHINI:
Inafikika umbali wa kilomita 145 kwa njia ya barabara kutoka hifadhi ya Taifa ya Serengeti,kilomita 60 kutoka hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara, na Kilomita 180 (maili 112) kutoka Mkoani Arusha. Ni mwendo wa saa 2 mpaka 3 kutoka Arusha. Saa 1 kutoka hifadhi ya ziwa Manyara na saa 2 mpaka 3 kutoka Serengeti. Hii ni hifadhi ambayo ipo katikati baina ya ziwa Victoria, ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika, na mlima Kilimanjaro, Mlima mrefu kuliko yote Afrika.

MAUMBILE ASILIA YA
KIJIOGRAFIA HIFADHINI:
Uwanda mpana wenye tambarare , milima, Milima yenye Volkano, na misitu yenye mandhari nzuri ya kupendeza.

HALI YA HEWA USAWA WA
BAHARI HIFADHINI:
Inaanzia mita 1500 mpaka 3600 kutoka usawa wa bahari.

VIVUTIO VIKUU VYA UTALII
HIFADHINI:
Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro crater), Bonde la Empakai, Mlima Oldoinyolengai, mlima pekee Tanzania ambao Volkano yake bado ni hai. Bonde la Oldupai, sehemu ambayo ndio chimbuko la historia yetu. Vile vile misitu yenye mandhari nzuri yenye kupendeza.
WANYAMAPORI WAPATIKANAO
HIFADHINI: Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro crater), Bonde la Empakai, Mlima Oldoinyolengai, mlima pekee Tanzania ambao Volkano yake bado ni hai. Bonde la Oldupai, sehemu ambayo ndio chimbuko la historia yetu. Vile vile misitu yenye mandhari nzuri yenye kupendeza.
Simba, Fisi, Nyumbu, Viboko, Swala Granti, Swala Tomi, Kongoni aina ya Cokei, Ngiri Wanyamapori, Pofu, Pundamilia, Duma, Mbogo (Nyati), Tembo Madume (Bonde la ngorongoro), Tembo majike na watoto nje ya bonde la Ngorongoro. Viumbe hai ndege ni pamoja na mbuni, Tandawala, Kanga na wengineo wengi. Vile vile ndio sehemu pekee zaidi Tanzania kuwaona wanyamapori aina ya faru zaidi katika bonde la Ngorongoro.
MAMBO YA KUCHUKUA:
Vifaa vyote muhimu vinavyohusiana na safari yenu ya matembezi hifadhini;

HUDUMA ZA MAHITAJI
MENGINEYO:
Mambo ya ziada ya mahitaji yanayojitokeza na upatikanaji wake katika sehemu husika.

UOTO WA ASILI HIFADHINI:
Uoto wa asili katika mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro inaangukia katika uoto wa asili wa milimani (Afro – Montane region) na uoto mwingineo tofauti tofauti kama vile tambarare zenye nyasi fupi (short grassy plains)

WAKATI WA KUTEMBELEA
HIFADHINI:
Mwezi wa Desemba mpaka Februari. Vile vile mwezi Mei mpaka Julai.

HUDUMA ZA CHAKULA:
Je mtakuwa na mpishi wenu? Au mtajibebea vyakula vyenu wenyewe? Kama ndivyo sivyo, Je huduma za chakula mtazipata wapi?

Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ipo karibu sana na
mji wa Karatu kwa upande wa Kusini ambapo
sehemu nyingi hupatikana zitoazo huduma za vyakula.
HUDUMA ZA MALAZI AU KULALA:
Safari yenu ya matembezi hifadhini ni lazima izingatie kama mtalala ndani ya hifadhi (kupiga kambi au mahema). Kama hamtalala ndani ya hifadhi, Je ni mpangilio na utartibu upi mtakaouandaa? Hii ndio dira itakayowapatia picha halisi ya mambo kama ni kubeba vifaa vya kupigia kambi au hapana. Kwa upande mwingine, nyumba za kulala wageni katika mji wa Karatu zinapatikana.

GHARAMA ZA USAFIRI WOTE:
Hii ndio dira elekezi itakayotoa picha halisi ya safari yenu ya matembezi hifadhini. Haya yote ni baada ya kukamilisha mambo kama vile maandalizi ya usafiri, huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo yatakayojitokeza kama vile dharura.

MAMBO YA KUFAHAMU:
Kama mtatumia usafiri maalumu wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kuteremkia katika bonde la ngorongoro basi kuna ulazima wa kuwepo mawasiliano kuweza kufahamu kama huduma hiyo ipo au haipo.Kama huduma hiyo haipo basi utaratibu mwingine uandaliwe. Kufahamu haya yote ni lazima kuwasiliana na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kama kuna uwezekano huo upo. Je ni Kampuni zipi nyinginezo mtakazozitumia zinazotoa huduma hiyo hifadhini?

MAMBO YA KUFANYA:
Watanzania watalii wa ndani ni vizuri wakaelimishana wao wenyewe
katika vikundi vyao kuhusiana na elimu ya huduma ya kwanza.

MAWASILIANO
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
S.L.P. 1, Ngorongoro
Simu; +255 27 253 7006
+255 27 253 7019
+255 27 253 7007
Nukushi;
+ 255 27 253 7007
Tovuti; www. Ngorongoro – Crater – africa.org.
Barua pepe; ncaa-info@africaonline.co.tz
ncaa-info@cybernet.co.tz
ncaafarm@cybertnet.co.tz)

MAMBO YA KUZINGATIA HIFADHINI:
Kanuni na taratibu za hifadhi ni muhimu sana kutekelezwa ili kuepuka matatizo ambayo yanayoweza kujitokeza.

Ukweli kuhusu Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro.
Ikumbukwe na Ieleweke hapa ya kwamba Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro si eneo ambalo ni hifadhi ya Taifa na vile vile eneo hili la ngorongoro halipo chini ya Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) na badala yake ni Shirika huru kama jinsi ilivyo TANAPA likijitegemea. Kazi na majukumu ya TANAPA na NGORONGORO zinafanana katika kuhifadhi viumbe hai na makazi yake kuwa endelevu kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo. Lakini kwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni eneo ambalo ni hifadhi mseto ambapo kuna viumbe hai aina tatu vikiishi kwa pamoja ambavyo ni watu ambao zaidi ni jamii ya Kabila la Wamaasai, mifugo yao kama vile Kondoo, Mbuzi na Ngombe na tatu ni Wanyamapori. - See more at: http://tazamaramanitanzania.com/Mamlaka%20ya%20Hifadhi%20Ngorongoro.html#.U32gPii57gk

0 comments:
Post a Comment