Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka mshindi wa kwanza kati ya
Wizara za Serikali zilizoshiriki katika Maonesho ya Nane Nane
yaliyofanyika Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Mbali na kuwa mshindi wa kwanza kati ya Wizara zote za Serikali ,
Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka kuwa mshindi wa Tatu wa jumla ya
Wizara, Taasisi na Mashirika yote yaliyoshiriki kwenye maonesho hayo.
Wizara ya Maliasili na Utalii ilikabidhiwa vikombe viwili na hati tatu
za ushindi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Nane Nane na Mgeni Rasmi,
Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Mhe. Stepheni Wassira
Aidha,. Imetunukiwa hati ya kuwa kati ya Wizara iliyoshiriki
kikamilifu kwenye maonesho hayo tangu siku yalipozinduliwa na hadi siku
ya kilele cha maadhimisho.
Licha ya ushindi huo , Wizara ya
Maliasili na Utalii ndio Wizara pekee iliyoongoza kwa kutembelewa na
wananchi wengi zaidi takribani elfu sitini kwa siku tangu maonesho
yalipoanza hadi siku ya kilele chake ukilinganisha na Wizara na Taasisi
zingine.
Mbali na Tuzo hizo , Wizara inajivunia kwa kuwawezesha
wadau wake watatu wanaojishughulisha na ufugaji nyuki walio chini ya
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kuibuka washindi kwa
kujipatia hundi za pesa na hati za ushiriki kwenye maonesho hayo.
Akizungumza kwenye Maadhimisho ya kilele cha Maonesho hayo Mgeni
Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rai, Mhe. Stephen Wassira aliipongeza
Wizara kwa kujituma na kujitolea kwa hali na mali kuhamasisha na
kuelimisha Wananchi wa Kanda ya kati katika masuala ya Uhifadhi na
ufugaji Nyuki wa Kisasa.
Alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ni
wadau muhimu sana na ni rafiki Kilimo hivyo ushirikiano huo ni lazima
uwe endelevu ili kutokomeza vita dhidi ya Ujangili kwa sabau Jangili
yeyote anayeingia kwenye hifadhi ni lazima apitie kwenye mashamba ya
wakulima ndio aingie kwenye Hifadhi hivyo ushirikaiano huu utafanya
vitendo vya ujangili kuisha kwa kuwa Wakulima watakuwa wakitoa taarifa
juu ya ujangili huo
Mhe. Wassira, alisisitiza kuwa maonesho
haya ni lazima yaoneshe tija kwa Wakulima kwa kuwainua kiuchumi tofauti
na ilivyozeoleka miongoni mwa watu kuwa Wakulima na wafugaji ni watu
maskini na hawakopesheki’’
‘’Wakulima na Wafugaji ni mtu muhimu
sana katika nchi hii hivyo ni lazima watengenezewe mazingira rafiki ili
waweze kufikia ndoto zao kwa kutumia teknolojia za kisasa’’ Mhe. Wassira
alisisitiza.
Alisema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha maisha
ya Wakulima na wafugaji tayari imeshaanzisha Benki ya Wakulima na
Wafugaji ili kuwawezesha kupata mikopo ili waweze kuendesha shughuli
zao kwa njia ya Kisasa.
Mhe. Wassira alisema serikali inafanya
kila liwezekanalo kuendelea kupima maeneo mbalimbali hapa nchini kwa
nia ya kuzuia mifakarano amabyo imekuwa ikiibuka kila uchao na
kusababisha vifo vya wananchi wasio na hatia.
Naye Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi alitoa wito kwa Wananchi kuchangamkia
fursa mbalimbali zinazopatikana katika Kanda kati hasa suala la kilimo
na kuachana na dhana iliyojengeka kuwa nyanda hizo ni ombaomba, tegemezi
na kame.
Kwa kumalizia Mhe Wassira aliwasihi Wananchi hasa
Wakulima na Wafugaji kuendelea kushirikiana serikali katika kutimiza
ndoto zao kwa kutumia njia za kisasa licha ya kuwa pembejeo zimekuwa
ghali na kusuasua kwa soko la mazao yao hivyo serikali inafanya kazi
usiku na mchana kuhakikisha changamaoto hizo zinakwisha.
0 comments:
Post a Comment