WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAZIDI KUTEMBELEWA KWENYE BANDA LAKE KATIKA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KATI MKOANI DODOMA

Wizara ya Maliasi;li na Utalii ikiwa ni wadau muhimu wa kutambua na kuthamini umuhimu wa siku ya Wakulima Kitaifa hivyo inashiriki kwenye Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati Mjini Dodoma
Ikiwa Leo ni Siku ya Nne Tangu yalipozinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu, Wananchi mbalimbali wamekuwa wakifurika kuja kujionea Utajiri ,kubwa tuliojaliwa pamaoja na kupewa elimu juu ya ufugaji nyuki.
Maonesho ya NaneNane yanafanyika Kanda saba nchini ambazo ni Kanda ya Kaskazini Arusha, Kanda ya Mashariki Morogoro, Nyanda za juu Kusini Mbeya, Kanda ya Kusini Lindi na Songea na Kanda ya Kati Dodoma,
Kwa mwaka huu Maonesho haya Kitaifa yanafanyika mkoani Lindi licha ya kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inashiriki Kanda ya Kati mjini Dodoma.
Hivyo basi Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa wito kwa Wananchi wote kuja kutembelea banda lake ili kuweza kujionea vivutio vya kitalii kama vile Simba, Chatu, nyoka Chui, Kobe wakubwa na Wadogo, Sokwe, Nyani,Kasuku, Duma , Ndege Karani, Fisi madoa, Fisi miraba,Tumbusi na Ndege wa kila aina, mbao na miche ya miti ya matunda na vivutio vingine vya asili.
Tenga muda wako sasa kwa kutumia fursa hii muhimu kutembelea viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma kuja kujionea vivutio vya Kitalii.


0 comments:

Post a Comment