Rais
Jakaya Kikwete, akikata utepe kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii
wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana , Wa tatu kulia ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi na
watatu pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Balozi Charles Sanga
akiwa ameshikilia utepe huo.
Rais
Jakaya Kikwete, akimpa mkono Afisa Mhifadhi wa Mambo kale, Bw.
Ngivingivi wakati alipotembelea Banda la Wizara Maliasili na Utalii
kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE)
Dar e s Salaam jana , Wa tatu ( Katikati) ni Afisa Mwandamizi wa Mambo
kale, Bw. Mwita akifurahia .
Rais
Jakaya Kikwete, akiwa ameshikilia zawadi wakati alipotembelea banda la
wadau wa Utalii kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa
ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana , Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi akisikiliza kwa
makini maelezo ya Mdau wa Utalii ( hayupo pichani)
Rais
Jakaya Kikwete, akifurahia kikundi cha ngoma kutoka Burundi
kikitumbuiza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya
Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana , Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi na wa tatu kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Balozi Charles Sanga akiangalia kwa makini
Wasanii hao ( hawapo pichani)
Rais
Jakaya Kikwete, akifurahia maelezo alipotembelea Banda la Wizara ya
Utalii la Burundi kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa
ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana , Wa pili kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi na wa tatu kulia
ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Balozi Charles Sanga wakisikiliza kwa
makini maelezo ( mtoa maelezo hayupo pichani)
Rais
Jakaya Kikwete, akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Bidhaa Mwanadamizi
wa Benki ya CRDB, Yustro Bituro ( kushoto) kuhusu matumizi maalumu ya
mashine ya kulipia mapato ya Utalii katika vituo vya kupokea watalii
nchini kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili
(S!TE) Dar e s Salaam jana.
Rais
Jakaya Kikwete, akisaini kitabu cha mahudhurio alipotembelea banda la
Wachina kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili
(S!TE) Dar e s Salaam jana
Rais Jakaya Kikwete, akihutubia kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja
Rais Jakaya Kikwete, akihutubia kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana.
Baadhi
ya Washiriki na waoneshaji wa maonesho wakimsikilza kwa makini Rais
Jakaya Kikwete, ( hayupo pichani) akihutubia kwenye ufunguzi wa Maonesho
ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akiwa
anamkaribisha Rais Jakaya Kikwete, ( wa pili ) kuhutubia kwenye
ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE) Dar e s
Salaam jana
Mhe. Rais Jakaya Kikwete, amesema kwamba Vyombo vya habari vya
Magharibi vimekuwa kikwazo kwa ukuaji wa Tasni ya Utalii Barani Afrika
kwa kuripoti habari hasi.
Aliyasema hayo jana wakati akifungua
Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili yajulikanayo kama Swahili
International Tourism Expo ( S!TE) yaliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya
Utalii yanayoendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo zaidi
ya nchi kumi na tano zinashiriki Maonesho hayo.
Mhe. Rais
alisema kwamba Vyombo vya habari vya Kimataifa vimekuwa vikijikita zaidi
kuripoti habari mbaya kuhusu Bara la Afrika kana kwamba Afrika hakuna
mazuri yoyote yanayofanyika na yaliyopo katika tasnia ya Utalii pamoja
MaliasIli zake.
‘’Afrika imekuwa ikiripotiwa kuwa ni bara la njaa, magonjwa, machafuko, vita na ukabila’’ Mhe. Rais alisisitiza, Kwa sasa ugonjwa wa Ebola umekuwa ndio ajenda kwa vyombo vya habari vya Kimataifa kana kwamba Ugonjwa huo umeenea nchi zote za Afrika kitu amabacho sio kweli, hivyo ni lazima tuukatae upotoshaji huu.
Alisema kwa kuwa vyombo vya Kimagharibi vimekuwa vikijikita kuielezea Afrika kama ni nchi moja badala ya kuuelezea Afrika kama Bara hivyo vyombo vya habari vya Afrika havina budi kuripoti habari chanya kuhusu Afrika ukizingatia uwepo wa vivutio vya Kiutalii vinavyopatikana Barani Afrika pekee.
‘’Afrika imekuwa ikiripotiwa kuwa ni bara la njaa, magonjwa, machafuko, vita na ukabila’’ Mhe. Rais alisisitiza, Kwa sasa ugonjwa wa Ebola umekuwa ndio ajenda kwa vyombo vya habari vya Kimataifa kana kwamba Ugonjwa huo umeenea nchi zote za Afrika kitu amabacho sio kweli, hivyo ni lazima tuukatae upotoshaji huu.
Alisema kwa kuwa vyombo vya Kimagharibi vimekuwa vikijikita kuielezea Afrika kama ni nchi moja badala ya kuuelezea Afrika kama Bara hivyo vyombo vya habari vya Afrika havina budi kuripoti habari chanya kuhusu Afrika ukizingatia uwepo wa vivutio vya Kiutalii vinavyopatikana Barani Afrika pekee.
Alisisitiza kuwa endapo Vyombo vyetu vya habari vitaielezea Afrika kuwa
ni sehemu nzuri ya kupumzika na kufurahia tofauti na inavyoripotiwa
kwa sasa, Kwa kufanya hivyo Watalii wengi watakuja kutalii na kujionea
vivutio vyetu.
‘’Maonesho hayo ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili ni hatua muhimu Mhe. Rais alisema, Mhe. Rais alisisitiza kuwa ,
‘’Maonesho hayo ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili ni hatua muhimu Mhe. Rais alisema, Mhe. Rais alisisitiza kuwa ,
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema licha ya jitihada kubwa zinazofanyika
kutangaza Utalii wa ndani na wa nje lakini Waongozaji wageni na Wakala
wa Huduma za Utalii wamekuwa kikwazo cha ukuaji wa Utalii nchini kwa
kuwa wamekuwa sio wakarimu kiasi cha kutosha nahivyo kuwafanya Watalii
wengi wanaokuja kutembelea vivutio vya kitalii kushindwa kufurahia
kutokana na huduma wanazopewa na hivyo kupeleka picha mbaya pindi
wanavyorejea makwao.
Ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
kushirikiana na Wadau wa Tasnia ya Utalii kushirikiana kwa pamoja
kutengeneza mazingira rafiki ya kuwafanya Wataliii kuja kutembelea
vivutio vyetu kwa kuongozwa na Waongozaji Watalii wenye weledi na
uzalendo wan chi yetu.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi alisema Wizara itazidi kuweka
Mazingira wezeshi ya kuwafanya Wazawa pamoja na wageni wanashirikiana
kwa pamoja kutengeneza miundo mbinu ya Kiutalii kwa nia ya kuwavutia
Watalii wengi zaidi kuja Nchini.
Alisema hadi sasa Wizara
inaendeleakuandaa mazingira ya kukuza Utalii wa Kiutamaduni ambapo kila
Kabila litapata fursa ya kutangaza Utalii wake na hivyo kila jamiii
husika itaweza kupata mapato yatakanayo na Utalii moja kwa moja tofauti
na sasa ilivyo.
Bi Maimuna Tarishi alitoa wito kwa Watanzania
wajitokeze kwa wingi kutembelea Maonesho hayo ya Kimataifa kwani ni
fursa adimu sana kwao hivyo waitumie ipasavyo kwa nia ya kupata elimu
pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali za kuwekeza kwenye Utalii kwa
kuwa ni sekta mtambuka.
Maonesho hayo yalianza juzi na yanatarajiwa kufungwa kesho ambapo yanatarajiwa kutoa kutoa elimu juu ya Utalii wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment