SHINDA SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI

Katika kutambua mchango wa Wananchi katika uhifadhi na kupiga vita ujangili wa wanyamapori na sekta ya misitu nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imeamua kuchezesha bahati nasibu ya kutembelea hifadhi za taifa.

Bahati nasibu hiyo itachezeshwa katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya SABASABA yatakayoanza kufanyika Juni 28 hadi Julai 10, mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere jijini Dar es Salam.

Katika bahati nasibu hiyo itakayochezeshwa kila siku, washindi mbalimbali watakaopatikana watazawadiwa safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Mikumi na Saadani na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii.

Aidha, zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi mbalimbali watakaoshiriki katika bahati nasibu hiyo.

Sambamba na hilo Wizara katika kuimalisha utalii wa ndani nchini imeandaa Safari za kila siku za gharama nafuu za kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Saadani ambapo mwananchi atagharamia usafiri wa kutoka viwanya vya Sabasaba hadi hifadhini na kurejea siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam

Wizara inatoa wito kwa wananchi wote kutembelea banda la Wizara ili kupata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale watakaokuwa wanatoa elimu juu ya jambo lolote la sekta husika.
CHANZO; Wizara ya Maliasili na Utalii


1 comment:

  1. Welcome to brotherhood Illuminati where you can become
    rich famous and popular and your life story we be change
    totally my name is Dan Jerry I am here to share my
    testimony on how I join the great brotherhood Illuminati
    and my life story was change immediately . I was very poor
    no job and I has no money to even feed and take care of my
    family I was confuse in life I don’t know what to do I try all
    my possible best to get money but no one work out for me
    each day I share tears, I was just looking out my family no
    money to take care of them until one day I decided to join
    the great Illuminati , I come across them in the internet I
    never believe I said let me try I email them.all what they
    said we happen in my life just started it was like a dream to
    me they really change my story totally . They give me the
    sum of $1,200,000 and many thing. through the Illuminati I
    was able to become rich, and have many industry on my
    own and become famous and popular in my country , today
    me and my family is living happily and I am the most
    happiest man here is the opportunity for you to join the
    Illuminati and become rich and famous in life and be like
    other people and you life we be change totally.If you are
    interested in joining the great brotherhood Illuminati.then
    contact him +2348106618681 or for more information +1(705)8062021
    email:illuminatibrotherpowerful@gmail.com or you need my assistance
    email:danjerry04@gmail.com...

    ReplyDelete