USIKOSE KUTEMBELEA BANDA LAKO NAMBA MOJA KATIKA MSIMU HUU WA SABASABA 2014

Wizara ya Maliasili na Utalii inashiriki kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya SABASABA mwaka huu yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere, Saba Saba, Barabara ya Kilwa.

Wizara inawakaribisha wananchi wote wenye kiu ya kuona na kuelimika kuhusu shughuli za Utalii, Ufugaji Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.

Ikumbukwe kuwa Banda la Maonesho la Wizara miaka yote huwavutia watu wengi wanaoshiriki katika maonesho ya Viwanda na Biashara hali ilinayowapelekea watu wengi kushindwa kuingia ndani kuona wanyama kutokana na umati mkubwa wa watu wanaofurika hasa inapokaribia kilele cha maonyesho.

Wizara inapenda kuwajulisha wananchi wanaopenda kujielimisha na kuona shughuli mbalimbali za Wizara kutembelea banda kuanzia Mwanzo wa maonyesho badala ya kusubiri siku ya ufunguzi ambapo watu hufulika kiasi cha wengi kushindwa kutii kiu zao wafikapo bandani.

Aidha, katika kuimalisha utalii wa ndani Wizara imeandaa safari za kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Saadani kwa gharama nafuu ikiwa ni gharama za usafiri kutoka viwanya vya Sabasaba hadi hifadhini na kurejea siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam.

Sambamba na hilo Wizara itachezesha bahati nasibu ambapo mshindi atakayeshinda atazawadiwa safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Mikumi na Saadani.
Wizara haijawasahau wananchi wanaopenda kutunza mazingira kwa kupanda miti ya matunda, kivuli pamoja na mapambo kwa kuhakikisha inawaletea miche mbalimbali bandani inayouzwa kwa bei nafuu.

Ndani ya banda wananchi watapata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale watakaokuwa wanatoa elimu juu ya jambo lolote litakalokuwa linamtatiza mwananchi aliyefika bandani hapo.

Miongoni mwa wanyamapori hai watakaokuwepo ni kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na mfalme wa pori SIMBA.
CHANZO CHA HABARI; Wizara ya Maliasili na Utalii


1 comment:

  1. Welcome to brotherhood Illuminati where you can become
    rich famous and popular and your life story we be change
    totally my name is Dan Jerry I am here to share my
    testimony on how I join the great brotherhood Illuminati
    and my life story was change immediately . I was very poor
    no job and I has no money to even feed and take care of my
    family I was confuse in life I don’t know what to do I try all
    my possible best to get money but no one work out for me
    each day I share tears, I was just looking out my family no
    money to take care of them until one day I decided to join
    the great Illuminati , I come across them in the internet I
    never believe I said let me try I email them.all what they
    said we happen in my life just started it was like a dream to
    me they really change my story totally . They give me the
    sum of $1,200,000 and many thing. through the Illuminati I
    was able to become rich, and have many industry on my
    own and become famous and popular in my country , today
    me and my family is living happily and I am the most
    happiest man here is the opportunity for you to join the
    Illuminati and become rich and famous in life and be like
    other people and you life we be change totally.If you are
    interested in joining the great brotherhood Illuminati.then
    contact him +2348106618681 or for more information +1(705)8062021
    email:illuminatibrotherpowerful@gmail.com or you need my assistance
    email:danjerry04@gmail.com...

    ReplyDelete