WAZIRI NYALANDU ATIA SAINI HATI YA UANZISHWAJI WA JUMUIYA ZA WANYAMAPORI ZA WAGA NA UMEMARUWA.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe .Lazaro Nyalandu ametia saini ya kuanzishwa kwa jumuiya za wanyamapori za Waga na Umemaruwa ikiwa ni ushirikishwaji wa jamii katika kulinda na kuhifadhi wanyamapori.
Hafla hiyo ya utiaji saini ilifanyika hivi karibuni Mpingo House jijin Dar es Salaam na kushuhudiwa na viongozi akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Selestin Gesimba na Wakuu wa Idara na vitengo.
Mhe. Nyalandu alisema uanzishwaji wa jumuiya hizo ni hatua mojawapo muhimu iliyofanywa na Wizara ikiwa ni njia mojawapo ya kuiwezesha jamii inayozunguka maeneo hayo kuongeza kipato kutokana watalii watakaokuwa wanatembelea maeneo hayo.
Aliongeza kuwa, Wananchi wanaozunguka maeneo hayo washiriki kikamalifu katika kulinda na khifadhi rasilimali za wanyamapori pamoja na kupambana na vitendo vya ujangili.
Aidha, Mhe. Nyalandu alielezea ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa Kasane, Botswana uliofanyika hivi karibuni kuwa umekamilika na kwamba ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Katika mkutano huo, Jumuiya ya Kimataifa imeipongeza Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi sita za kwanza, kuanza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa London wa Februari 2014, alisema Mhe. Nyalandu
Mhe. Nyalandu aliongeza kuwa katika mkutano huo Tanzania iliungana na Botswana, Chad, Gabon , Ethiopia na Kenya katika kuanzisha mpango wa’’ Elepaht Protectve Iniative’’ EPI, na jitihada hizo ziliongozwana na Mwana Mfalme wa Uingereza Prince Charles, zinaendelea kutekelezwa kwa nchi kupiga marufuku biashra ya meno ya tembo katika kipindi cha miaka kumi.
Alisisitiza kuwa kutokana na ushawishi wa Tnzania, nchi za Malawi na Uganda zimekubali kujiunga na Mpango wa ‘’Elelphant Protection Initiative’’ EPI.
Mhe. Nyalandu aliongeza kuwa Wizara yake imeshachukua hatua za kulinda na kuhifadhi akiba ya Taifa ya meno ya tembo, inayofikia tani 130,000, tayari Tanzania na Uingereza zimeanza utekelezaji wa mapango wa ‘’STOP IVORY’ wenye lengo la kufanya uhakiki wa akiba ya meno ya ya tembo nchini, na kutenegenza mfuko wa kisayansi wa kuhifadhi na kuyalinda.


0 comments:

Post a Comment