(Chini ya Sheria ya Misitu namba 14 ya mwaka 2002 ambayo pia
inatambulika kama Sheria ya Misitu Sura Namba 323 (RE: 2002). Na
ifahamike Kwamba;
1. MSITU WA HIFADHI WA MIKOKO (MANGROVE FOREST
RESERVE) UMEHIFADHIWA KISHERIA KWA TANGAZO LA SERIKALI LA MWAKA 1928 NA
SHERIA ZA TANGANYIKA ZA MWAKA 1947 SURA YA 132 UKURASA WA 1346 IKISOMWA
PAMOJA NA SHERIA YA MAZINGIRA YA MWAKA
2004 VIFUNGU VYA 52 (a) NA 54 (b), SHERIA YA ARDHI NAMBA 4 YA MWAKA 1999
KIFUNGU CHA 7 NA SHERIA YA MATUMIZI YA ARDHI NAMBA 8 YA MWAKA 2008
KIFUNGU CHA 28.
2. MTENDAJI
MKUU WA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) KWA KUSHIRIKIANA NA
NEMC NA WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI ANAWATAARIFU NA
KUWATANGAZIA WATU WOTE WALIOVAMIA MSITU WA HIFADHI WA MIKOKO NA KUISHI
NA KUFANYA SHUGHULI ZOZOTE ZA KIBINADAMU, KUWA SHUGHULI WANAZOZIFANYA
NDANI YA MSITU HUO NI KINYUME CHA SHERIA YA MSITU NAMBA 14 YA MWAKA 2002
(FOREST ACT NO. 323 (RE: 2002).
3. KWA TAARIFA HII, MNATANGAZIWA KUWA MMEVUNJA SHERIA YA MISITU NAMBA 14 YA MWAKA 2002 KIFUNGU CHA 26 (g), (h) NA 84 (1) (b), (2), (3).
4. KWA MUJIBU WA SHERIA YA MISITU ILIYOTAJWA HAPO JUU, MNATAKIWA KUSITISHA SHUGHULI ZENU ZOTE NA KUONDOKA KATIKA MSITU WA HIFADHI WA MIKOKO KATIKA KIPINDI CHA SIKU SABA (7) KUANZIA TAREHE YA TANGAZO HILI.
5. YEYOTE ATAKAYEKAIDI MAELEKEZO YALIYOMO KWENYE TANGAZO HILI, ATAONDOLEWA KWA NGUVU NA VYOMBO VYA DOLA PAMOJA NA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
6. PIA ATAKAYEKAIDI KUTOKA KWA HIYARI YAKE MWENYEWE, ATAWAJIBIKA KULIPA GHARAMA ZITAKAZOTOKANA NA ZOEZI LA KUWAONDOA KWA NGUVU, KWA KULIPA FIDIA ZA UHARIBIFU WA MSITU.
7. TAFADHALI ZINGATIENI KUWA, HATUA HIZO HAPO JUU ZITACHUKULIWA MARA MOJA BAADA YA SIKU SABA (7) (IFIKAPO TAREHE 7/01/2016) ZA TAARIFA HII KUMALIZIKA KUANZIA TAREHE 31 DESEMBA, 2016.
8. TANGAZO HILI LINAZINGATIA ILANI NA AMRI ZOTE ZILIZOWAHI KUTOLEWA NA VIONGOZI PAMOJA NA VIKAO MBALIMBALI KUHUSU UHIFADHI WA MSITU WA MIKOKO.
Juma S. Mgoo
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA

0 comments:
Post a Comment