KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AKABIDHIWA JANA OFISI RASMI NA ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO, DKT. ADELHELM MERU AMBAYE KWA SASA KAHAMISHIWA WIZARA NA VIWANDA NA BIASHARA.

 Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( kulia) akikabidhiwa taarifa ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Adelhelm Meru jana tarehe 04 Januari 2016 ambaye kwa sasa kahamishiwa Wizara ya Viwanda na Biashara (kushoto ) ofisini kwake Mpingo House.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi watumishi wa ofisini kwake mara baada ya kukabidhi ofisi hiyo kwa Katibu Mkuu wa sasa, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( hayupo pichani)
 Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru ( wa pili kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Bi. Anjelina Madete ( wa kwanza kushoto) mara baada ya makabidhiano ya taarifa ya ofisi Mpingo House jijini Dar es Salaam. Wengine ni Katibu Muhtasi Bi Mariam Malunga ( katikati ) pamoja na Mtumishi Bi. Judith ( wa kwanza kushoto)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ( katikati) akizungumza ofisini kwake Mpingo House na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) wakiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Bi. Anjelina Madete (kulia) maara baada ya kuwasili Wizarani hapo tayari kwa kutekeleza majukumu yao.


0 comments:

Post a Comment