Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) inautaarifu umma kwa ujumla hususan wafanyabiashara na watumiaji wa mazao ya misitu kuzingatia yaliyomo kwenye ,Sheria ya Misitu Namba 14 ya mwaka 2002 ambayo pia inatambulika kama
Sheria ya Misitu Sura Namba 323 (RE: 2002), Kanunina Miongozo inayoelekeza taratibu za
uvunaji, usafirishaji na jinsi ya kufan ya biashara ya mazao ya misitu. Sheria na Kanuni inaelekeza yafuatayo:
1.Kila mvunaji wa mazao ya misitu
lazima awe na leseni halali ya uvunaji wa mazao ya misitu iliyotolewa na
mamlaka husika. Aidha, kila gunia la mkaa lililobebwa na chombo chochote cha
usafiri ni lazima liwe limekatiwa risiti halali ya malipo ya serikali;
2. Kila msafirishaji wa mazao ya
misitu lazima awe na kibali (Transit Pass -
TP) cha kumruhusu kusafirisha mazao
ya misitu ikionyesha mahali mazao hayo yalipotoka na yanapokwenda ikiambatishwa
na leseni ya uvunaji;
3.Kila mfanyabiashara lazima awe
amesajiliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuwa ni mfanyabiasharahalali
wa mazao ya misitu;
4.Usafirishaji wa mazao ya misitu ni
kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni;
5.Ni marufuku kusafiriksha mkaa kwa
kutumia pikipiki zinazotumia matairi mawili
6.Bishara ya Mkaa lazima ifanyike
katika maeneo maalum yaliyoanishwa katika kila wilaya;
7.Ni marufuku kwa wafanyabiasha ya
mkaa kufanya biashara hiyo kandokando ya barabara;
8.Kwa wanunuzi wote wa mkaa kwaajili
ya matumizi ya Kaya ni lazima wawe na risiti halali ya serikali inayoonesha
malipo yaliyofanyika kwa idadi ya magunia ya mkaa aliyonunua;
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa
kwa yeyote atakayekiuka utaratibu huu.
Imetolewa na:
Juma S. Mgoo
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA-D’SALAAM
16 Desemba, 2015





0 comments:
Post a Comment