Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza
katika kikao na Idara ya Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara
hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Januari, 2015.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika kikao na Idara ya
Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House
Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Januari, 2015.
Kamu
Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Bi. Gladnes Mkamba (wa pili kulia)
akiwasilisha taarifa ya Idara yake kwa Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe wa (pili kushoto) katika kikao hicho.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Juma Mgoo
(kulia) akiwasilisha taarifa ya ofisi yake kwa Waziri wa Maliasili
na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kulia).
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe.
Sehemu ya wajumbe katika kikao hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza katika kikao hicho.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amemsimamisha
kazi Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu
wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo na
Maofisa wa Misitu wa Mikoa nchi nzima kupisha uchunguzi wa upotevu wa
mapato ya Serikali.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo Dar
es Salaam, Prof. Maghembe amesema agizo hilo limekuja kutokana na
ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali
yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa
kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Ameagiza pia maofisa hao wote wanaokusanya maduhuri ya Serikali
katika Wilaya watumie muda wa siku kumi kuanzia leo kuhakikisha maduhuri
yote yaliyokusanywa yanapelekwa benki ikiwa ni pamoja na kukabidhi
vitabu vya kukusanyia mapato kinyume cha hapo watachukuliwa hatua kali
za kisheria.
“Wale district forestry officers wote wapeleke vitabu vyao
wanavyokusanyia maduhuri ya Serikali kwenye ofisi za Kanda, Naibu Katibu
Mkuu tusaidie kuwasiliana na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ifanye
ukaguzi wa vitabu hivyo ndani ya siku kumi tuhakikishe fedha
zinazotakiwa zinaingia kwenye mfuko wa Serikali, Mtu anakusanya fedha
ya Serikali toka mwaka 2004 mpaka leo hajapeleka benki ananeemesha hali
yake ya nyumbani, hili hapana”. Alisisitiza Prof. Maghembe.
Kwa mujibu wa Waziri Maghembe Bw. Mohammed Kilongo ambaye Idara yake
ndiyo inatoa vitabu kwa ajili ya kukusanya maduhuri ya Serikali katika
Mikoa yote na Wilaya zote nchini analazimika kusimamishwa kazi kupisha
uchunguzi ambapo ukikamilika sheria itachukua mkondo wake bila uonevu
wowote.
Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amewaagiza
pia Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kutumia muda wa siku saba
kurudi katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii maarufu kama Mpingo
House ambalo walihama mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka jana na kwenda
kupanga katika jengo la NSSF Mafao House lililopo Ilala.
“Wakati tunajenga nyumba hii hapa, tumejenga jengo hili ni kama jengo
la misitu ndio maana linaitwa Mpingo House kwa maana ni jengo la
Misitu, ninyi wenyewe mmejenga jengo kubwa hili mmemaliza mmehama,
Naagiza jumatatu Desemba 11 muwe mmesharudi katika jengo hili, ghorofa
ya tatu nikija kukagua niwakute, haiwezekani mueleze matatizo yote
mliyonayo muhame nyumba ya Serikali mkapange jengo hapo jirani” Alisema
Prof. Maghembe.
Katika hatua nyingine ya kuboresha uhifadhi wa Misitu nchini Waziri
Maghembe ameiagiza Idara ya Misitu na Nyuki ya Wizara ya Maliasili
kuhakikisha inajiimarisha katika lengo lake kuu la uhifadhi kwa
kushirikiana na wadau wanaohusika kuhakikisha Mamlaka iliyolengwa ya
Uhifadhi Misitu inakamilika.
“Tunataka tutoke kwenye Wakala wa Huduma za Misitu (Tanzania Forestry
Services Agency) twende kwenye Mamlaka ya Uhifadhi wa Misitu (Tanzania
Forestry Services Authority) ili tuweze kufanya vizuri zaidi kwenye eneo
la uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini, Katibu Mkuu tunaomba pia
usaidie kufanikisha hili” Alisema Prof Maghembe.
Aliongeza kuwa wakati wa kuundwa Mamlaka hiyo ni vizuri pia Idara ya
Misitu na Nyuki ya Wizara ya Maliasili ikatenganishwa na kila moja kuwa
Idara kamili kutokana na umuhimu wa kila sekta katika kujenga uchumi wa
nchi kwa kutoa fursa ya kuboresha maeneo hayo na kuongeza pato la taifa.
Ameitaka pia Idara ya Misitu na nyuki kupitia Wakala wa Huduma za
Misitu (TFS) kuhakikisha kuwa inaongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali
kwa kuziba mianya yote ya ubadhilifu pamoja na kuanzisha vyanzo vipya
vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo.
Akizungumzia mchango wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwenye pato
la taifa Mtendaji Mkuu, Bw. Juma Mgoo amesema katika mwaka huu wa fedha
TFS imeweka makisio ya kukusanya Tsh. Bilioni 88 ambapo mpaka hivi sasa
wameshakusanya zaidi ya asilimia 20 na makisio hayo.
Waziri Maghembe akizungumzia kuhusu uvamizi kwenye hifadhi za taifa
na mapori ya akiba amewataka wananchi wote waliovamia maeneo ya hifadhi
za taifa kwa ajili ya kuchunga mifugo waondoke ndani ya siku saba
zijazo, na wale walivamia mapori ya akiba kwa shughuli za kilimo na
ufugaji waondoke ndani ya miezi mitatu ijayo.
“Serikali itawaondoa kwa nguvu wasipotekeleza agizo hili la kuondoka
katika maeneo ya hifadhi za taifa na kwenye mapori ya akiba
yaliyohifadhiwa” Alisisitiza Prof. Maghembe.
Akizungumzia kuhusu biashara ya Mkaa, Prof. Maghembe amewaagiza wataalamu wa Idara ya Misitu kusimamia biashara ya mkaa kwa kuzingatia taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji wa Mkaa nje ya nchi.
Akizungumzia kuhusu biashara ya Mkaa, Prof. Maghembe amewaagiza wataalamu wa Idara ya Misitu kusimamia biashara ya mkaa kwa kuzingatia taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji wa Mkaa nje ya nchi.
Ameongeza kuwa nishati ya Mkaa ni muhimu lakini Tanzania ina hifadhi
kubwa ya makaa ya mawe ambapo ameitaka Idara ya Misitu kwa kushirikiana
na wadau wengine kuona ni namna gani ya kuweza kutumia mbadala huo kwa
kuzalisha makaa hayo ya mawe kwa matumizi ya kawaida ili kuokoa misitu
nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri yatafanyiwa kazi kwakuwa lengo lake ni kuona dhamira ya msingi ya Serikali ya awamu ya tano inafikiwa ya kubana matumizi, kuongeza mapato ya Serikali na kuhifadhi maliasili za taifa ikiwemo misitu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri yatafanyiwa kazi kwakuwa lengo lake ni kuona dhamira ya msingi ya Serikali ya awamu ya tano inafikiwa ya kubana matumizi, kuongeza mapato ya Serikali na kuhifadhi maliasili za taifa ikiwemo misitu.





0 comments:
Post a Comment