Bodi ya Utalii Tanzania imeibuka mshindi wa tatu miongoni mwa Bodi za utalii bora barani Afrika katika shindano lililoendeshwa na tasisi ya Kimarekani iitwayo Travvy (Travvy Awards) na kutunukiwa tuzo ya bronze.
Bodi ya Utalii ilikuwa miongoni mwa nchi tatu zilizoingia fainali
katika kundi la Bara la Afrika. Bodi nyingine mbili zilizoingia katika
nafasi bora tatu ni za Afrika ya Kusini na Namibia ambapo Afrika ya
kusini iliibuka mshindi wa kwanza ikifuatiwa na Namibia.
Akizungumzia ushindi huo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii
Tanzania Bi Devota Mdachi alisema ushindi huu unaonyesha jinsi gani
tunajituma na kufanya kazi kwa weledi licha ya changamoto kadhaa
zinazotukabili. “Ushindi huu ni kielelezo kwamba tunafanya kazi nzuri
pamoja na changamoto kadhaa tulizo nazo” alisema Bi Devota. Aliongeza
kuwa nafasi ya tatu tuliyoipata imetupa faraja na kututia hamasa sana na
huu ni ushindi wa nchi na wadau wote wa sekta ya utalii kwa ujumla.
SOURCE;TTB
0 comments:
Post a Comment