PMU YAIMARIKA ZAIDI
Hongera kitengo cha PMU kupata wafanyakazi wapya. Ndugu.Edrick Jackob na Reuben Lameck karibuni sana kwenye familia ya TTB.
Na: Ripota wetu
Kitengo cha manunuzi cha Bodi ya Utalii Tanzania kimeongezewa nguvu
zaidi baada ya wafanyakazi wawili kuhamishiwa Bodi ya Utalii kutoka
maeneo mengine ya utumishi serikalini.
Wafanyakazi hao Bw. Edrick Jakob Kipanda ambaye ni Afisa Ugavi darala
la kwanza aliyejiunga na TTB akitokea Wizara yana Umwagiliaji. Bw.
Kipande ana shahada ya Uzamili katika Manunuzi na Menejimenti ya Ugavi
kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe wakati Bw. Reuben Lameck Bhokeye ambaye ni
Afisa Ugavi Mwandamizi amejiunga na TTB akitokea idara yaTaifa ya
Takwimu. Bw Reuben ana Stashahada ya juu ya Manunuzi.
“Najisikia raha sana na amani sana moyoni kwa kupata watumishi hawa
wawili katika kitengo changu na hii imenipa ari zaidi ya kazi” alisema
mkuu wa kitengo hicho Bi Mcharo huku akitabasamu alipoulizwa na ripota
wa TTB habari kuhus namna anvyojisjikia kuongezewa nguvu mpya katika
kitengo chake.
Kabla ya hapo kitengo hicho kilikuwa na wafanyakazi wawili Maria Hamson na Alice Mcharo ambaye ni mkuu wa kitengo hicho.
MBWAMBO NA MSHANA WASTAAFU RASMI KAZI
Na: Ripota wetu
Utumishi wa Umma wa wafanyakazi wa siku nyingi Bibi Rose Waridi
Mbwambo na Bw. Amani Yohane Mshana umefikia kikomo baada ya watumishi
hao kustaafu kazi rasmi hivi karibuni.
Bw. Msahana na Bibi Mbwambo ambao walikuwa waajiriwa wa Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) wameitumikia Bodi kwa muda mrefu toka ilipokuwa
Shirika la Utalii Tanzania (TTC) na hatimaye Bodi ya Utalii Tanzania.
Bi Rose Mbwambo aliyekuwa mkuu wa kituo cha habari za Utalii cha TTB
kilichokuwa mtaa wa Samora jijini Dar es salaam aliajiriwa mwaka 1994
kama Afisa Habari za Utalii na kuendelea kupanda mpaka kufukia Afisa
Habari za Utalii Mwandamizi (Senior Tourist Information Officer) cheo
ambacho amekitumikia mpaka anastaafu tarehe 17/11/2015
Naye Bw. Amani Johane Mshana aliajiriwa na Bodi ya Utalii Tanzania
mwaka 1996 kama dreva na alifanya kazi katika tawi la Arusha ambako
aliendelea kupanda cheo na kufikia ngazi ya dreva Mwandamizi nafasi
ambayo amehudumu kuhudumu mpaka alipostaafau rasmi tarehe 31/12/2015.
TTB YAPOKEA WANAFUNZI KWA AJILI YA MAFUNZO KWA VITENDO
Na: Ripota wetu
Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wameendelea kupata
nafasi ya kujifunza kwa vitendo (practical) Bodi ya Utalii Tanzania
katika idara na vitengo mbalimbali baada ya kupata mafunzo yao kwa njia
ya ndaharia wawapo vyuoni.
Hivi karibuni TTB imepokea wanafunzi wawili Happy Boniface Choma wa
mwaka wa kwanza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) anayesoma
kozi ya Menejimenti ya Raslimali watu (Human Resoursce Management). Bi
Happy Choma ambaye yuko katika idara ya Utawala na Raslimali watu
atakuwa TTB kwa mafunzo mpaka mwezi Machi 2016.
Mwanafunzi mwingine ni Happy Mchekelo Lenis wa Chuo cha VETA Mtwara
anayesomea Ukatibu Muhutasi naye atakuwa hapa mpaka Machi 2016 akiwa
chini ya Bi Hidaya Kayera.
Bodi ya Utalii imekuwa na utaratibu wa kutoa fursa kwa wanafunzi
kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini kujifunza kwa vitendo kozi
wanazosomea katika vyuo wanavyotoka.
WAWILI WAAJIRIWA TTB KWA MKATABA WA MUDA
Na: Ripota wetu
Katika kuimarisha utendaji wake na kuboresha wa huduma izitoazo kwa
wadau mbalimbali wa ndani ya shirika na nje, Bodi ya Utalii Tanzania
imeajiri vijana wawili kwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja kila mtu.
Watumishi hao ambao wako katika ajira ya muda toka tarehe 09/11/2015
wote wanahudumu upande wamapokezi (reception) na kabla ya kujiunga na
TTB walikuwa katika maeneo mengine ya utumishi na chuoni.
Bi Zainab Lugwani ambaye ana cheti cha Front office operation kutoka
chuo cha Taifa cha Utalii (National college of Tourism) amejiunga na TTB
akitokea katika hotel ya Blue pearl iliyopo ubungo ambako pia alikuwa
upande wa mapokezi. Nae Bi Husna Mohammed amejiunga na TTB akitokea
masomoni chuo cha Taifa cha Utalii ambako alihitimu stashahada ya Front
office operation. Kabla ya hapo Bi Husna alifanya kazi Msalaba Mwekundu
(Red Cross Tanzania) akiwa ni mtunza stoo (store keeper).
BODI YA UTALII TANZANIA YAWANIA TUZO YA MWAKA YA KIMATAIFA YA WORLD TRAVEL AWARDS
Na: Ripota wetu
Bodi ya Utalii Tanzania ni miongoni mwa taasisi na vivutio 24 vya
utalii vya Tanzania vulivyoingizwa kwa ajili ya kuwapata washindi wa
Annual World Travel Awards (AWT) kwa makundi (categories) mbalimbali
katika sherehe ya utoaji tuzo hizo ambazo mwaka huu zitafanyika April 9
mwaka huu Zanzibar katika hotel ya Diamonds La Gemma dell’Est
Bodi na Mamlaka nyingine za Utalii zinazoshindanishwa na TTB katika
chini ya Destination category katika kundi la Bodi zinazoongoza Africa
kwa mwaka 2016 ni pamoja na Mamlaka ya Utalii ya Misri, Bodi ya Utalii
ya Gambia, Mamlaka ya Utalii ya Ghana, Bodiya Utalii ya Kenya, na
Shirika la Taifa la Utalii la Morocco. Mengine ni Bodi ya Utalii ya
Namibia, Shirika la Maendeleo ya Utalii la Nigeria na Kamisheni ya
Utalii ya Zanzibar.
Taasisi nyingine na vivutio vya utalii kutoka Tanzania vilivyoingizwa
kuwania tuzo hizo na makundi yao katika mabano ni Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Julius Nyerere, Bandari za Dar es salaam na
Zanzibar, Zanzibar kama eneo la utalii, Mlima Kilimanjaro, Bonde la
Ngorongoro, na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Nyingine ni hotel ya Diamond La Gemma dell’Est, Hoteli ya Dream of
Zanzibar na Hideaway of Nungwi Resort &Spa, Hoteli za Blue bay Beach
Resort & , Dream of Zanzibar, Karafuu Beach Resort &Spa na
Diamond La Gemma dell’Est zote za Zanzibar: Serena Hotel –Dar es salaam;
Singita Sasakwa Lodge; Breezes Beach Club na Karafuu Beach & Spa;
Beyond Mnembe Island Lodge na Chapwani Private Island: Four Season
Safari Lodge Serengeti; Singita Sabora Camp na Jongomero Camp.
Upigaji kura umeanza Februari Mosi mwaka huu na umefikia mwisho Februari 29, 2016.
Imetolewa Na:
Mhariri Mkuu TTB HABARI.
Simu: +255222127424
Mobile: +255 713 439 928
Tuandikie:
BODI YA UTALII TANZANIA
Utalii House — Mtaa wa Laibon / Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Karibu na ubalozi wa Ufaransa
S.L.P 2485
Dar es Salaam, Tanzania
0 comments:
Post a Comment