WARSHA YA KUSIMAMIA MABADILIKO ( CHANGE MANAGEMENT TEAM-CMT)YA UANZISHWAJI WA MAMLAKA YA UHIFADHI WANYAMAPORI TANZANIA (TANZANIA WILDLIFE MANAGEMENT AUTHORITY-TAWA), TAREHE 29- 09,2014 HADI 4-10,2014

Baadhi ya Kikosi Kazi cha Kusimamia Mabadiliko kutoka Idara ya Wanyamapori kwenda TAWA (Change Management Team-CMT).
 Mmojawapo wa Washiriki wa Warsha, Bw. Mvungi akichangia hoja kuhusu masuala ya TAWA
 Hoteli ya Oceanic Bay mjini Bagamoyo ambako Warsha ya kuhusu TAWA ilikofanyika.
 Baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo wakisiliza kwa makini mada kuhusu TAWA kutoka kwa Mtaalamu Elekezi Bw. Frank Kretzschmar kutoka GIZ ( hayupo pichani)
 Afisa Wanyamapori Mkuu, Bw. Twaha Twaibu akizungumzia masuala ya mawasiliano kwenye Warsha hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya TAWA wakiwa kwenye picha ya pamoja mjini Bagamoyo
Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2011 ilianzisha Kikosi Kazi kilichopewa jukumu la kuratibu mchakato wa kuanzisha Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Authority-TAWA). Kikosi kazi hiki kiliandaa Amri (Order) ambayo imebeba mwongozo wa kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori. Awali zilikuwa zimeandaliwa rasimu za Sheria za uanzishaji wa Mamlaka na Idara ya Wanyamapori ambapo baadaye ilishauriwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuwa ni vema Mamlaka ikaanzishwa kwa Amri. Kwa Amri hiyo TAWA ilianzishwa rasmi kwa amri kusainiwa na Mhe. WMU tarehe 9 Mei 2014.

Aidha, Februari 2014, Idara ya Wanyamapori iliwateua Maafisa Wanyamapori saba kuungana na wajumbe wa kikosi kazi hiki kuunda kikosi cha Kusimamia Mabadiliko (Change Management Team-CMT). Kazi kubwa ya kikosi hiki ni pamoja na kuwaandaa watumishi katika ngazi mbalimbali kutoa mafunzo kwa ajili ya kukabilianana na mabadiliko na kuandaa Mpango mkakati wa mabadiliko ya Idara ya Wanyamapori Kwenda TAWA
Kikosi cha mabadiliko kimeandaa rasimu ya Mkakati wa Mabadiliko ya Idara kwenda Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania pamoja na mpango wa muda mfupi wa kuwezesha utekelezaji wa mpango mkakati wa mabadiliko kwa muda wa miezi sita. Mpango huu wa muda mfupi unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika lake la GiZ.
Warsha hii imeanza rasmi leo tarehe 29/09/2014, mjini Bagamoyo na itamalizika tarehe 4/10/2014. Dhumuni kubwa la Warsha hii ni mwendelezo wa maandalizi ya kuboresha rasimu ya mkakati wa mabadiliko na kuanda Mpango kazi wa TAWA na kuwaanda watumishi katika ngazi mbalimbali kutoa mafunzo kama ilivyoelezwa hapo awali.
Warsha hii inajumuisha Maafisa mbalimbali nchi nzima kutoka katika Mapori ya Akiba, Vikosi Dhidi ya Ujangili na Malihai Clubs of Tanzania. Warsha hii inafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika lake la GiZ Chini ya Mtaalamu elekezi Bw. Frank Kretzschmar.Tutaendelea kuwafahamisha mchakato wa warsha hii unavyoendelea. SOURCE: Ministry Of Natural Resources and Tourism


0 comments:

Post a Comment