Inaijua Kampeni Maalum ya kutangaza Utalii Iliyozinduliwa na Rais Kikwete? Hii hapa...

 
Ministry of Natural Resources and Tourism - Tanzania's photo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete. alizindua kampeni maalum ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mtandao na kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Katika uzinduzi huo, Rais Kikwete aliwapongeza Mhe. Lazaro Nyarandu , Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt, Adelhelm Meru na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii. Bi. Devota Mdachi kwa kuandaa mtazamo mpya wa kutangaza vivutio vya Utalii katika Nyanja za kimataifa.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika Kilimanjaro Hoteli , jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali, wadau wa uhifadhi pamoja na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara Mhe. Rais Dkt. Jakaya alisema vivutio vya Utalii vilivyopo nchini ni muhimu kutangazwa ili viweze kufahamika kwa kupitia tangazo la ‘’Tanzania ni roho ya Afrika’’ ( Tanzania is the soul of Tanzania) itasaidia kufahamika kimataifa.
Alisema tangazo hilo litaanza kurushwa kwenye Televisheni ya Kimataifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC na CCN kwa nia ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini katika Nyanja za Kimataifa.
‘’Uamuzi wa kuvitumia vituo ya CNN na BBC ni mzuri sana kwa sababu huko ndiko kuna watalii wengi wanaokuja Afrika na Tanzania’’ Mhe. Kikwete alisema
Aliongeza kuwa Tanzania imo katika nchi tano Afrika na nchi 52 duniani ambazo zinapata wageni zaidi wanaokuja kutembelea hifadhi zetu
Alisema Sekta ya Utalii ili iweze kukua inahitaji uwekezaji mkubwa katika matangazo kwa kufanya hivyo Watalii wengi zaidi wataweza kuja kujionea vivutio tulivyonavyo.
Rais Kikwete alisema anajisikia fahari kuzindua tangazo hilo lililoandaliwa kwa ustadi wa hali ya juu litakaloiwezesha Tanzania kufahamika Ulimwenguni pote kutokana Utajiri uliojariwa nao.
Alisema Matangazo ni muhimu sana katika sekta ya Utalii kwa kuwa yanawafanya Watalii wa Kimataifa kuvutiwa na kuamua kuja kutembelea vivutio vyetu pasipo matangazo hakuna watalii watakaojua vivutio tulivyo navyo.
‘’Sekta ya Utalii ndani ya kipindi changu cha uongozi imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sasa ndo sekta ya kwanza kwa kuliingiza Taifa pesa za kigeni kwa kiasi cha shilingi billion mbili ikifuatiwa na sekta ya madini’’ ‘’ Tumepiga hatua kubwa licha ya kuwa bado kuna changamoto zinazohitaji kushughulikiwa.’’ Rais Kikwete alisema.
Aliongeza, Sekta ya Utalii kwa sasa inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na kwamba jitihada zinazoendelea kufanywa na viongozi ni ishara kuwa kazi inafanyika na itaendelea kufanyika.
Rais Kikwete alisema uamuzi wa kutayarisha tangazo hilo inadhihirisha ubunifu na utayari wa viongozi na watendaji na kwamba, ana imani kubwa litaongeza kasi ya watalii kuja nchini
‘’ Nakupongeza sana Mhe. Lazaro Nyalandu kwa uamuazi wako huu ni sahihi na utakuwa chachu ya kukuza na kuvitangaza vivutio vyetu kikamilifu sekta ya Utalii itaendelea kuwa kinara katika kuchangia pato la taifa.’’
Aidha alisema sekta ya Utalii imekuwa ya pili kwa kutoa ajira kwa Watanzania ikiongozwa na sekta ya Kilimo hivyo kwa kupitia tangazo hilo jipya lililozinduliwa itazidi kuajiri vijana wengi zaidi kwa siku za usoni.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu alisema kampeni hiyo inalenga kukuza sekta ya Utalii nchini ambayo ni moja ya mkakati wa kufikiwa na malengo ya millennia.
‘’ Mhe. Rais unaondoka madarakani ukiwa umeacha vitu vya kukusemea katika sekta ya Utalii kwani katika kipindi chako imeitendea haki’’ Alisema Nyalandu.
Pia Mhe. Nyalandu alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Kikwete kutokana kutumia muda wake mwingi wa mapumziko kuliko viongozi waliomtangulia kwa kutembelea mbuga za wanyama nchini.
Kutokana na kutambua mchango wake, Shirika la Hifadhi la Taifa ( TANAPA) limempa zawadi maalum ya kutembelea bure hifadhi kwa muda wote yeye na familia yake.
Imempa zawadi ya picha ambayo alipiga akiwa akiwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Kinyago kama ishara ya kuthamini mchango wake katika kuhamasisha Utalii nchini
 
 


0 comments:

Post a Comment