AJALI YATOKEA MLIMA KILIMANJARO

TAARIFA KWA UMMA
AJALI YA MAPOROMOKO KILIMANJARO YAUA MMOJA

Leo majira ya saa kumi alfajiri kumetokea ajali ya maporomoko ya mawe katika eneo la juu la Mlima Kilimanjaro la Hans Meyer na kusababisha kifo kwa mwanafunzi Malata Thomas kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli .
Aidha, mwanafunzi mwingine Matenga S.J alivunjika mguu wake na anaendelea na matibabu katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.
Wanajeshi hawa walikuwa pamoja na wenzao 265 walikuwa katika mafunzo yao ya kawaida ya ukakamavu katika Mlima Kilimanjaro.

Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea na taratibu za kufahamu chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo na taarifa kamili itatolewa kwa umma mara baada ya kukamilika.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano kwa Umma
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
15.07.2014


0 comments:

Post a Comment